Skip to product information
1 of 1

MZALENDO KIMATHI by Ngūgī wa Thiong'o & Mīcire Gīthae Mūgo

MZALENDO KIMATHI by Ngūgī wa Thiong'o & Mīcire Gīthae Mūgo

Regular price KSh500.00
Regular price Sale price KSh500.00
Sale Sold out
Shipping calculated at checkout.

Mengi yameandikwa juu ya kiini cha mapambano baina ya Mau Mau na vikosi vya wakoloni Waingereza. Je, kiini hiki kimezungumziwa vya kutosha katika fasihi ya Kenya? Kwa nini fasihi hii imewadunisha wazalendo na kuwafanya wasioweza kuiunda historia yao? Kwa nini waimbaji wetu Kenya hawajapata kuimba nyimbo za kuwasifu mashujaa kama Dedan Kimathi na ujasiri wao? Historia na matendo waliyoyaandika wanahistoria na waandishi wengine ni ya nani? 

Haya ni baadhi to ya maswali yaliyowafanya Ngugi wa Thiong'o na Micere Githae Mugo kuandika mchezo wa Mzalendo Kimathi, mchezo wa aina ya pekee unaoonyesha mapambano ya Kenya katika harakati za kujikomboa. Mhusika mkuu ni Kimathi, kiongozi shupavu wa mapinduzi ya Mau Mau. ingawa anateswa kwa aina nyingi, Kimathi anagoma kabisa kujisalitisha na Ubeberu wa Waingereza. 

View full details